Licha ya kuonekana na madansa wa kike katika jukwaa la Fiesta 2014 Mwanza, Diamond anasema hajabahatika kumpata dansa wa kike mwenye vigezo anavyovitaka.
“Sina
madansa wa kike pale wawili ni wa Vanessa naweza sema wote si wangu,
zamani nilikuwa na madansa wa kike, lakini kwa sasa Tanzania tuna
upungufu kwenye muziki wa Bongo Fleva na muziki wa bendi kuna madansa
ambao wamebobea kucheza muziki wa dansi pekee. Nilitamani kuwa na
madansa wa kike zamani lakini ilishindikana maana kuwapata ni ngumu
sana,” anasema na kuongeza:“
Mpaka
sasa bado natafuta madansa wa kike sijawapata, nahitaji dansa wa kike
ambaye anajua, awe anajiamini afuatilie madansa wa nje wanachezaje, awe
na unyamwezi kidogo ni ngumu sana, awe mbunifu afuatilie muziki wa nje
na vitu kama hivyo. Kwa hiyo nikatamani nifanyaje nikaamua kuazima
madansa wa watu nifanye nao shoo,” anasema.
No comments:
Post a Comment