Licha ya kuonekana na madansa wa kike katika jukwaa la Fiesta 2014 Mwanza, Diamond anasema hajabahatika kumpata dansa wa kike mwenye vigezo anavyovitaka.
“Sina madansa wa kike pale wawili ni wa Vanessa naweza sema wote si
wangu, zamani nilikuwa na madansa wa kike, lakini kwa sasa Tanzania tuna
upungufu kwenye muziki wa Bongo Fleva na muziki wa bendi kuna madansa
ambao wamebobea kucheza muziki wa dansi pekee. Nilitamani kuwa na
madansa wa kike zamani lakini ilishindikana maana kuwapata ni ngumu
sana,” anasema na kuongeza:
“Mpaka sasa bado natafuta madansa wa kike sijawapata, nahitaji dansa wa
kike ambaye anajua, awe anajiamini afuatilie madansa wa nje wanachezaje,
awe na unyamwezi kidogo ni ngumu sana, awe mbunifu afuatilie muziki wa
nje na vitu kama hivyo. Kwa hiyo nikatamani nifanyaje nikaamua kuazima
madansa wa watu nifanye nao shoo,” anasema.
Akiwazungumzia madansa wake wa kiume ambao ni sita, Diamond anasema ni
madansa wanaolipwa pesa ndefu ukilinganisha na madansa wote Afrika
Mashariki.
"Siwezi kusema nawalipa kiasi gani itakuwa kama nawavua nguo, lakini
hakuna madansa wanaolipwa vizuri kama wangu Afrika Mashariki, ikiwa bei
inaongezeka na mimi nawaongeza katika malipo yao. Wako sita kwa kweli
nimetoka nao mbali tangu ‘Kamwambie’ mwaka 2009, nimekua nao kifikra,
kiumri na kiakili na kuona kwamba hawa ni mzigo wangu mimi na wanafanya
kazi pamoja na mimi, wale ni mafanikio yangu wana msaada mkubwa sana
pengine nisingekuwa hapa bila wao,” anasema.
Hata hivyo, anaweka wazi kwamba linapofika suala la shoo za nje, huwa
inategemea ni wapi kwani shoo zingine hairuhusiwi kwenda na madansa wote
hivyo huwa anawabadilisha kwa zamu.
Katika
mahojiano hayo maalum na Mwananchi, superstar huyo alisema kuwa kwasasa
muziki wa Bongofleva unakubalika nje ya nchi tofauti na zamani.
No comments:
Post a Comment