FIGO KATIKATI YA SHABANI RAMADHANI NA NSAJIGWA
|
Kikosi cha wakongwe wa Real Madrid kimewaonyesha soka wakongwe wa Tanzania kwa kuwachapa mabao 3-1.
Mabao ya Real Madrid, yote matatu yalifungwa na Ruben de la Red ambaye alianza kufunga moja katika kipindi cha kwanza.
Lakini Tanzania Eleven wakasawazisha baada ya Roberto Rojas kujifunga wakati akijaribu kuokoa.
Kipindi cha pili, De la Red akafunga mengine mawili, moja likiwa la mkwaju wa penalty.
Luis Figo ndiye alikuwa kivutio zaidi kwa mashabiki wengi waliojitokeza kwenye uwanja huo.
Mashabiki wengi walikuwa wakimshangilia wakati akiwahenyesha mabeki Shadrack Nsajigwa, Mecky Maxime na Salum Sued.
Madrid ndiyo walikuwa kivutio zaidi kutokana na kucheza kwa kuonana zaidi.
Pasi zao zilikuwa za uhakika kuliko kikosi hicho chini ya Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
DE LA RED AKIKABWA NA ATHUMANI CHINA NA HABIB KOND
|
Hata
hivyo, safu ya ushambuliaji ya Tanzania Eleven iliyoongozwa na Madaraka
Selemani na Kali Ongala ilionekana kutokuwa na makali sana.
Ongala, Sabri Ramadhani ‘China’ na Athumani ‘China’ ndiyo walionyesha uhai zaidi katikati.
Lakini bado wasingeweza wenyewe hivyo kufanya kuwe na ugumu.
Mwisho,
Rais Kikwete aliwakabidhi kombe Madrid ikiwa ni ishara ya kushinda
mechi hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya TSN na kudhaminiwa na makampuni
kadhaa kama Sapphire Court Hotel, Fast Jet, Bin Slum Tyres, Championi na
TSN yenyewe.
CHANZO :SALEHE JEMBE
No comments:
Post a Comment