NAHODHA wa Arsenal, Thomas Vermaelen amejiunga na Barcelona kwa dau la
Pauni Milioni 15 baada ya timu hiyo ya Kaskazini mwa London kugoma
kuwauzia silaha wapinzani wa Ligi Kuu England, Manchester United.
Beki
huyo Mbelgiji amesaini Mkataba wa miaka mitano na vigogo hao wa
Hispania, ambao unaaminika utamfanya awe analipwa Pauni 80,000 kwa wiki.
Vermaelen
amekuwa Arsenal kwa miaka mitano na miaka miwili akiwa Nahodha wa
kikosi cha Arsene Wenger, lakini msimu uliopita alijikuta anawekwa
benchi Laurent Koscielny na Per Mertesacker.
No comments:
Post a Comment