Mario
anakubalika: Balotelli alikutana na mashabiki née ya viwanja vya
Melwood baada ya mazungumzo ya uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC
Milan
KLABU
ya Liverpool imemuahidi maslahi mazuri Mario Balotelli ili kuhakikisha
mshambuliaji huyo mtata anapiga mzigo wa uhakika Anfield.
Baada ya Liverpool
kukubali kutoa Pauni Milioni 16 za ada ya uhamisho kwa AC Milan kumnunua
nyota huyo, ilifanya kikao kizito na Mino Raiola, wakala wa mchezaji
huyo, Balotelli alikwenda mjini Manchester jana kufanyiwa vipimo vya
afya na baadaye akakutana uso kwa uso na kocha wa Liverpool, Brendan
Rodgers kwa mara ya kwanza.
Mamia
ya mashabiki wa Liverpool yalimlaki wakati anaondoka kwenye viwanja vya
mazoezi, Melwood na hakuna shaka atakapata mapokezi mazuri Anfield.
Mshambuliaji
huyo wa Italia atasaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya awe
analipwa Pauni zisizopungua 85,000- au 90,000 kwa wiki. Lakini
ameahidiwa marupurupu zaidi iwapo atafanya vizuri kazini.
Mamia ya mashabiki yalijitokeza kumshangilia Balotelli
Hapa ni wakati Balotelli anawasili Melwood kwa mazungumzo
No comments:
Post a Comment