02 August 2014

Njemba zaligombania penzi la JOKATE

jokate
Baada ya hivi karibuni mwanamitindo Jokate Mwegelo kutangaza kutafuta mchumba, idadi kubwa ya wanaume wamekuwa wakihaha kusaka mawasiliano naye huku kila mmoja akijinadi kivyake.
Mara baada ya habari ya Jokate ya kutafuta mchumba kutoka kwenye gazeti hili wiki iliyopita, namba ya simu ya chumba chetu cha habari imekuwa bize kupokea simu za wanaume mbalimbali wakiomba kuunganishwa na mrembo huyo.
Hata hivyo, jitihada za kumuunganisha mmoja mmoja kwa mrembo huyo hazikufanyika ila kwa yoyote anayehisi ana vigezo na ana nia ya dhati ya kumuoa na si kumchezea afike katika ofisi zetu nasi tutamuelekeza njia sahihi ya kumpata.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname