09 August 2014

MUME NA MKE WAZUA VARANGATI KISUTU

  Polisi wakimdhibiti jamaa huyo.

TIMBWILI! Jamaa mmoja na mkewe ambao wote hawakujulikana majina mara moja wamezua varangati la aina yake mahakamani kisa kikiwa ni kufutiwa kesi na kushindwa kuheshimu amri za maafande.Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar baada ya mume huyo kufutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya unyayasaji wa watoto wake wa kuwazaa. 
Jamaa huyo na mkewe walizua timbwili hilo wakati mtuhumiwa huyo akitolewa chumba cha mahakama kwenda kuweka sawa nyaraka ili awe huru. 

Huku akiwa na hasira, mwanaume huyo alianza kuzozana na polisi huku akiungwa mkono na mkewe wakikataa kutii amri ya askari aliyekuwa akiwaelekeza kwenda chumba kingine ili kukamilisha taratibu za kuwa huru.SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname