Boss wa Manchester United Louis van Gaal amesema itakuwa "maajabu" kama timu yake itashinda ligi kuu ya England msimu huu.
United wanacheza na Sunderland Jumapili, - baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Swansea.
Van
Gaal, 63, anajaribu kurekebisha kikosi "kisicho na uwiano", huku klabu
hiyo ikigoma kabisa kuzungumzia uhamisho wa Angel Di Maria kutoka Real
Madrid.
"Kushinda ligi msimu huu itakuwa maajabu. Lakini sisemi kuwa haiwezekani," amesema Van Gaal.
Kocha huyo Mholanzi amesema wamiliki wa Man United wanafahamu kuwa itakuwa "vigumu sana" kushinda ligi msimu huu.
"Nadhani familia ya Glazer wanafahamu hilo, vinginevyo nisingekubali kuchukua kazi hii," amesema.
Van Gaal alisaini mkataba wa miaka mitatu Old Trafford baada ya kumaliza kukiongoza kikosi cha Uholanzi katika Kombe la Dunia.
Alishinda
ligi katika msimu wa kwanza akiwa Barcelona na Bayern Munich, lakini
anaamini meneja yoyote anatakiwa kutazamwa katika msimu wa pili.
No comments:
Post a Comment