Mpiga
picha Evan Schiller na Lisa Holzwarth wametumia muda wao wa kutosha tu
kuchukua picha za tukio la kusisimua na kusikitisha huko Botswana baada
ya kushuhudia nyani mwenye mtoto akikumbana na hasira za simba jike
mwenye njaa ambaye alimfukuza na hatimaye kumkamata na kumuua.
Nyani
huyo aliuawa huku mtoto wake mchanga akiwa amemkumbatia pasipokujua
kuwa mama yake tayari alikuwa ameshakufa. baada ya simba kuua nyani huyo
sasa kibao alikigeuzia kwa mtoto ambapo aliaanza kumtisha pamoja na
mtoto huyo wa nyani kutaka kukimbia simba alimkamata tena. chanzo tabianchi
Baadae mtoto wa nyani alianza kucheza na simba na kumfanya kama mamayake. Tazama picha uone tukio kamili hatua kwa hatua.
Muda mfupi, mtoto wa nyani alitaka kutoroka lakini alishindwa kupanda mti, sasa simba akamfuata kuona nini kinaendelea.
Lakini cha ajabu badala ya simba kumuua mtoto huyo wa nyani alianza kucheza naye na kukafanya kanyani kasahau machungu.
hapa sijui nyani mtoto anawaza nini, weee usicheze na simba jamani.
Wacha
weee, sasa hapa simba sijui ndo kamsamehe kweli huyu nyani au ndo
amemuweka kiporo njaa ikiuma amtafune, lakini mtoto wa nyani anaonekana
kuenjoy tu.
Nyani mtoto kashapagawa na joto la simba, anaanza kutafuta kunyonya kifuani kwa simba, ana hatari huyu mtoto.
Raha iliyochanganyikana na hofu, hatari tupu
Wasije
simba wengine! simba jike akaanza kuwatimua sasa sijui alikuwa
anakalinda katoto ka nyani kasiliwe au aliona wenzake watammalizie msosi
wake wa baadae.
Haa!
kumbe baba nyani alikuwa kando akifuatilia issue yote na wakati simba
wanazinguana akapata upenyo wa kumuokoa mwanaye na kupanda nae kwenye
mti, uuuh kweli kama siku yako haijafika unaweza hata kumkamua maziwa
simba na akabaki kukuchekea tu
Stori
hii ni ya kufurahisha, huzunisha na kushangaza na inaonyesha ni kwa
kiasi gani kila jambo limepangwa kwa maksudi yake na kwamba hata tukiwa
katika magumu ya hali gani ukombozi unaweza kupatikana kikubwa tu ni
kujiamini kama mtoto wa nyani alivyofanya.
No comments:
Post a Comment