Baada
ya gari la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’
kukamatwa na polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la
ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama, amezungumzia nini kinaendelea
kwenye madai hayo.
Akizungumza
na Bongo5 leo, Dude amesema kuwa ni kweli gari yake imedaiwa kuhusishwa
na tukio hilo lakini uchunguzi unaendelea wa kuwatafuta wahusika
aliyokuwa amewaachia gari hilo.
“Siwezi kulizungumzia suala hili kwa sababu uchunguzi unaendelea na polisi, lakini gari yangu inadaiwa kukamatwa kwenye tukio la ujambazi,” amesema. “Kuna madogo walikuwa nayo hiyo gari, kwasababu nilikuwa naiuza kwahiyo hao madogo ndio walikuwa nayo. Lakini siwezi kulizungumzia suala hili kwa sababu kuna mtu wanamtafuta mpaka wamkamate ndo tujue hii kweli ilikuwaje. Kwahiyo kulielezea hili naonekana kama naharibu upelelezi wa polisi. Mimi hawakunikamata nilienda kwa sababu waliniita nikaenda kutoa tu maelekezo nikaachiwa. Sema tu gari yangu imeharibiwa kwa sababu wale vijana walipiga kelele za wizi wananchi wakabonda bonda lile gari. Nadhani kuanzia Jumatatu au Jumanne ninaweza nikalielezea hili kwa mapana zaidi kwa sababu nitakuwa nimeshajua polisi wanaendeleaje.”
Gari ya Dude
Kwa
mujibu wa Global Publisher, gari hilo lilihusishwa na tukio la ujambazi
linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21
mwaka huu ni aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ. Lilikutwa
likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif
Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za
usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
No comments:
Post a Comment