Wema akiwa na Diamond
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za
mauzo nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi
kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu
Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka
hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es
Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia
hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie
harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu
kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu
ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani
waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa
sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta
umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya
Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema:
“Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili
wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda
mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana
vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na
kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali
huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi
kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma
sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu
siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi
kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao
nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi
yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha
baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake
huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini
hatujaachana na hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu
No comments:
Post a Comment