07 August 2014

BALAA TUPU: WAREMBO WACHEZEA KICHAPO KIKALI BAA..KISA?! FUATILIA ZAIDI HAPA...!

 Akilia baada ya kula kichapo.
BALAA! Siku chache tu baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo wawili ambao majina yao hayakufahamika haraka wamejikuta wakila kichapo kutoka kwa mabaunsa kufuatia kuchelewa kutoka ndani ya baa waliyokuwa wakipombeka. Tukio hilo la aina yake lilijiri Agosti 5, mwaka huu katika baa hiyo mpya iliyopo Sinza ya Afrikasana jijini Dar es Salaam.

 Ilidaiwa kuwa, warembo hao waliambiwa mapema kuwa ifikapo alfajiri wasionekane kwenye eneo la baa hiyo lakini wao waliendelea kupombeka  mpaka jua linachomoza ndipo mabaunsa walipowaondolea uvivu kwa kuwapa kipigo. Mmoja wa warembo hao ambaye alionekana kukerwa na kitendo cha mwenzake kupigwa hadi kutokwa damu aliwalalamikia mabaunsa hao kuwa hawajawatendea haki kwa kuwafukuza kama mbwa na kipigo juu.SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname