BAADA ya
kuibuka sintofahamu kati ya waigizaji wa Bongo Movies, Salum Mchoma
‘Chiki’ na Vincent Kigosi ‘Ray’, Chiki ameibuka na kuzungumzia ishu
hiyo. Akipiga
stori mbili tatu na paparazi wetu, Chiki alisema kuwa yeye na Ray
hawakuwahi kuwa na bifu kama inavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii
isipokuwa walipishana kauli kidogo katika bethidei ya muigizaji Mahsein
Awadh ‘Dk. Cheni’ iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar
lakini waliyamaliza.
“Sina bifu na Ray tuko poa, pale Lamada tulipishana maneno kidogo tu ila kwa sasa stori kama kawa hatuna bifu la aina yoyote,” alisema Chiki.
“Sina bifu na Ray tuko poa, pale Lamada tulipishana maneno kidogo tu ila kwa sasa stori kama kawa hatuna bifu la aina yoyote,” alisema Chiki.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Salum Mchoma ‘Chiki’.
Kwenye
bethidei hiyo, ilidaiwa kuwa Chiki aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alimpa
maneno ya ‘madongo’ kumsisitiza atoe mkwanja ‘fedha’ nyingi kama zawadi
kwa Dk. Cheni hali ambayo ilimuudhi Ray.

No comments:
Post a Comment