Watu
wenye silaha wameua watu saba wakiwemo maafisa wanne wa polisi baada ya
kushambulia basi la abiria katika kaunti ya Lamu kwenye mwambao wa
Kenya.
Watu hao walishambulia basi hilo kwa risasi karibu na mji wa Witu, takriban kilomita 50 kutoka Lamu.
Baadaye walishambulia gari la polisi lililofika katika eneo la tukio.
Basi
hilo lililoshambuliwa siku ya Ijumaa lilikuwa likisafiri kutoka Mombasa
kwenda Lamu. Watu hao walishambulia basi hilo baada ya kuziba njia na
gari lao.
Dereva
wa basi ni miongoni mwa waliouawa, amesema kamishna Miiri Njenga wa
kaunti ya Lamu akizungumza na shirika la habari la Reuters.
Watu wanane wamelazwa hospitali, wengi kwa majeraha ya risasi.
Shambulio
hili limekuja siku moja baada ya jeshi la Kenya kusema ndege yake
imeteketeza kambi zinazotumika na kundi hilo katika eneo hilo.
Msemaji Wa al-Shabab, Abdulaziz Abu Musab, ameiambia Reuters kuwa tangazo hilo la Kenya ni "propaganda".
Kuhusu
shambulio la Ijumaa, amesema ni "kujibu madai ya Kenya kuwa imepeleka
wanajeshi wengi katika eneo la pwani na kuimarisha usalama".
Mamia
ya familia zimekimbia makazi yao katika maeneo hayo kutokana na
kutetereka kwa hali ya usalama ambayo pia imeathiri sekta ya utalii.
No comments:
Post a Comment