MUIGIZAJI mwenye jina katika filamu za Bongo, Kajala
Masanja juzi kati alipatwa na mchecheto ghafla wakati wa shughuli
iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere maarufu
kama Steve Nyerere huko Masaki, jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo ambalo Steve Nyerere alikuwa ameandaa chakula cha
usiku kwenye ukumbi wa Great Wall, MC wa shughuli, Chiki Mchoma alimtaka
Kajala kusimama na kutoa neno kwa niaba ya wasanii wa kike wa Bongo
Movie, lakini cha ajabu, mwanadada huyo alipatwa na aibu ya ghafla kiasi
cha kushindwa kuzungumza.
“Ni ajabu kweli yaani, maana Kajala tunayemjua siyo wa kushindwa
kusema kitu sehemu kama hii, halafu sasa alishindwa hata kutoa sababu
kwa nini hakuongea,” alisema msanii mmoja aliyekataa jina lake kuandikwa
gazetini
No comments:
Post a Comment