KONGWE wa
muziki wa kizazi kipya, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ameibuka na kufunguka
kuwa siri ya kufilisika kwake ni kupenda kwake sifa kutoka kwa wapambe
na matumizi mabaya ya fedha alizokuwa akiziingiza.
Akizungumza
na paparazi wetu, Nice, aliyetamba kwa staili ya Takeu, alisema wakati
nyota yake ikiwa juu na kuingiza pesa nyingi kutokana na kupata shoo
nyingi, alikuwa akitembea na kundi la mabaunsa, akibadilisha wanawake na
kufanya matumizi makubwa yasiyo na lazima kwa lengo la kutaka sifa.
“Enzi
zangu nani asiyejua kuwa nilikuwa natembea na kundi la mabaunsa, mademu
na kila kumbi nikiingia basi kila mtu atajua kama Nice yuko ndani
lakini mwisho wa sifa zile ni nini? Si ndiyo zimenifikisha hapa nilipo.
“Nilikuwa
na kila aina ya kamati ya ufundi, mashehe, wachungaji na maaskofu, wote
walikuwa wangu, lakini kwa kuwa nilikuwa nataka sifa, dua zao zilikuwa
kazi bure kwa sababu nilikuwa mtu wa starehe,” alisema Mr. Nice.
NENO LAKE KWA DIAMOND
Katika kile kinachoonekana kama kumuonya staa wa sasa anayekimbiza katika Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’, alisema kwa kila ‘vurugu’ anayoifanya, yampasa kumtazama yeye kama mfano halisi endapo ataendekeza maisha ya anasa na kutaka sifa.
Katika kile kinachoonekana kama kumuonya staa wa sasa anayekimbiza katika Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’, alisema kwa kila ‘vurugu’ anayoifanya, yampasa kumtazama yeye kama mfano halisi endapo ataendekeza maisha ya anasa na kutaka sifa.
“Diamond
kwa sasa anawika, anakubalika sana, ni kama ilivyokuwa kwangu. Namsihi
asijisahau. Maisha yanabadilika. Namtakia mema ndiyo maana namshauri.
Aachane na maisha ya kuwafurahisha watu, atengeneze maisha yake yajayo.
“Kuna
wakati muziki unakataa, hapo ndipo mawekezo yake yatakapomfanya
aendelee kuishi maisha bora bila muziki,” alisema Mr. Nice.
No comments:
Post a Comment