MPEJA BLOGKOCHA
wa AC Milan, Filippo Inzaghi anasema klabu hiyo ya San Siro inatakiwa
kuboreshwa idara zote kama inataka kuingia kwenye ushindani msimu wa
2014/2015.Milan
walifungwa mabao 5-1 na Manchester City katika mchezo wa kirafiki siku
ya jumapili baada ya kupoteza mechi nyingine kwa mabao 3-0 dhidi ya
Olympiacos na Inzaghi amegundua kuwa wanakabiliwa na kazi kubwa
kuiboresha timu kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi.
“Hili
lipo mbele ya macho ya kila mtu kwamba tunatakiwa kujiboresha idara
zote. Hatujafanya vizuri, tunatokea katika nafasi ya nane msimu
uliopita. Tunatakiwa kujiboresha mno,” Inzaghi aliiambia tovuti rasmi ya
Milan.
“Hatukucheza
vibaya sana dakika 10 za mwanzo. Tulicheza vizuri kwenye umilikaji wa
mpira na tulipopoteza mpira tulikosa mipango kabisa. Niliumia kwasababu
tulifungwa mabao mawili wakati tayari tulishatengeneza nafasi”.
“Bila mpira tulikuwa wabovu, tunatakiwa kupambana zaidi tunapopoteza mpira. Nahitaji kuona uwezo zaidi wakati hatuna mpira,”.
“Kazi
pekee ndio itatufanya tuingie katika ushindani mapema. Ni kazi yangu
kuiangalia tena mechi hii halafu kumuomba kila mtu anayehusika. Nadhani
tutakapokuwa kundi lililokamilika, tutaweza kuwa washindani katika
ligi”.
“Nimechukia
sana kwasababu kama kiwango ndio hiki, lawama zote ni kwangu na
wenzangu, lazima turekebishe. Tutarudi katika mstari wetu. Tunatakiwa
kufungwa mabao machache. Lazima tujiboreshe juu ya hili”.
Inzaghi siku za karibuni alitajwa kuwa kocha wa Milan baada ya Clarence Seedorf kufukuzwa kazi mwishoni mwa msimu wa 2013/2014.
No comments:
Post a Comment