Mwimbaji
wa kike Dayna Nyange azungumzia jinsi alivyokutana na changamoto nyingi
baada ya kuamua kubadili rangi ngozi yake na kuwa nyeupe.
Dayna
ameeleza kuwa amekuwa akisolewa na watu wengi huku wengine wakitumia
lugha mbaya dhidi yake lakini yeye ameipokea vizuri kwa kuwa anaamini ni
watu wanaompenda.
Ni
sawa kwa sababu mimi naamini ni watu wangu wa karibu na ni watu ambao
wananipenda ndio maana wanakuwa wanasema japo wengine wanatumia kauli
mbaya. Lakini pia ni sawa kwa sababu mimi najua hao ni binadamu na kila
binadamu anajua jinsi ya kupresent kwa mtu vile ambavyo anajisikia kwa
hiyo ni mimi kutumia tu akili nakipokeaje.
Amesema Dayna Nyange.
Ameeleza
kuwa yeye anaamini hakuna kitu ambacho aliwahi kukifanya kabla kikawa
gumzo au tatizo kwa watu na ndio maana watu wanaamua kulichukulia hili
kama tatizo kubwa.
Mwimbaji
huyo alitangaza uamuzi aliouchukua kufuatia changamoto hizo alizokutana
nazo ingawa anaamini kila mtu anauhuru wa kufanya maamuzi kama
alivyoamua yeye.
Kwa
hiyo mimi naweza kusema ni sawa, inawezekana kweli nimekosa. Lakini
mimi kama binadamu pia nina maamuzi yangu na nina sababu nyingi tu za
kufanya kile ninachokifanya. Japo nimesikia maneno mengi sana mpaka
Lol..’nimeacha.!
Siwezi
kusema kuwa nimeacha kabisa lakini nimetoka kule nilikokuwa, sasa hivi
narudi kuwa Dayna yule ambaye mnataka awe. Japo pia binadamu pia mnakitu
kimoja, sifieni kile kilicho bora kabla hakijakuwa sio.
Ameaongeza.
No comments:
Post a Comment