Stori: Gladness Mallya
STAA wa filamu Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ hivi
karibuni aliwachana wasanii wa kike na kuwataka kuachana na tabia ya
kulia na kuzimia kinafiki kwenye misiba kwani wanaonesha picha mbaya
katika jamii.
Wasanii wa Bongo Muvi na wadau mbalimbali wakiomboleza kifo cha Msanii mwenzao Recho.
Akizungumza siku moja kabla ya mazishi ya aliyekuwa msanii wa filamu,
Sheila Haule ‘Recho’, Cloud alisema baadhi ya wasanii wa kike wamekuwa
na tabia ya kulia kinafiki kwenye misiba.
“Sitaki
kwenye mazishi ya Recho kumuona msanii yoyote akijiangusha baada ya
kuona kamera za waandishi eti wamezimia jamani tuwe wastaarabu na kama
ukilia uwe unaumia kweli lakini siyo kinafiki kwani wasanii wa kike
wamekuwa na tabia ya kujiangusha huku wakiwaomba marafiki zao
wawaangalizie simu zao,” alisema Cloud.
MMH MAJANGA
ReplyDeleteSIOWA KIKE TU MBONA HATA HUYOMNAEMWITA MWENYEKITI WA BONGO MUVI ANALIA KINAFIKI.SHIN NAKAGAWA
ReplyDelete