Chumba cha kulala: Nyota wa
Ureno, Joao Moutinho ameposti picha hii kwenye mtandao wa Twita
akionesha chumba chake cha kulala nchini Brazil.
WAKATI kitu cha kwanza
atakachokiona Lionel Messi kila aamuka asubuhi ni mchezaji mwenzake
Sergio Aguero baada ya wawili hao kupangiwa chumba kimoja cha kulala,
Cristiano Ronaldo kwake ni tofauti kwani ataishia kuiona picha yake
kufuatia kupewa chumba cha peke yake.
Pengine hili litakuwa jambo
jema kwa Ronaldo aliyeshangilia bao la nne la Real Madrid kwenye fainali
ya UEFA baina ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid kwa kuvua jezi
yake na kutunisha kifua chake.
Moutinho (kushoto) ana matumaini ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Ureno kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ujerumani.
Mwanasoka bora wa dunia,
Cristiano Ronaldo (kulia) alicheza kwa dakika 66 katika mechi ya
kirafiki waliyoshinda mabao 5-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland
Ureno waliwasili katika kambi
yao na kukuta wameshaandaliwa vyumba vya kulala vikiwa na majina ya
wachezaji na kikosi kwenye vitanda vyao, pia kumewekwa picha zao
ukutani.
Kiungo Joao Moutinho na beki
Joao Pereira wote kwa pamoja wameposti picha za vyumba vyao kwenye
mtandao wa Twita na Instagram wakifurahia kabla ya kucheza mchezo wao wa
ufunguzi wa kundi D dhidi ya Ujerumani mjini Salvador juni 16.
Licha ya wasiwasi uliotanda
juu ya Ronaldo kukivaa kikosi cha Joachim Low baada ya kusumbuliwa na
majeruhi ya mguu aliyoipata kwenye mechi za UEFA, nyota huyo mwenye
miaka 29 ameonekana kuimarika hasa baada ya kucheza kwa dakika 66 kwenye
ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ireland siku ya jumatano.
Baada ya mechi ya Ujerumani,
vijana wa Paulo Bento watakabiliana na Marekani juni 22 mjini Manaus,
kabla ya kucheza mechi ya mwisho ya makundi mjini Brasilia dhidi ya
Ghana juni 26.
Hoteli ya Argentina kwenye
kombe la dunia ilipangwa mapema wiki hii, huku ikionesha wachezaji gani
watakuwa wanalala chumba kimoja wakati wote wa mashindano.
Mpangilio unaonesha kuwa washambuliaji Messi na Aguero watakuwa wanalala chumba kimoja.
Anajisikia nyumbani: Joao Pereira pia aliposti picha hii inayomuonesha akicheza mpira (kulia)
Chumba kimoja: Orodha ya wachezaji wa Argentina watakaokuwa wanalala chumba kimoja wakati wa fainali za kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment