Bara la
Afrika leo alfajiri limetupa karata yake ya pili kwenye michuano ya
kombe la dunia, kwenye mchezo kati ya Ivory Coast vs Japan.
Mchezo
huo ambao ulianza majira ya saa 10 usiku, umeisha kwa Ivory Coast kuitoa
kimasomaso Afrika kwa kuwa timu ya kwanza kushinda kwenye michuano ya
mwaka huu baada ya kuitungua Japan 2-1.
Magoli ya Ivory Coast yamefungwa na Wilfred Bony na Gervinho – Keisuke Honda aliifungia Japan goli la kufutia machozi.
Mchezo mwingine kwenye kundi hilo ulichezwa mapema kiasi saa mbili usiku kati ya Colombia dhidi Ugiriki.
Matokeo yalikuwa 3-0 kwa ushindi wa Colombia ambayo ilimkosa staa wao Radamel Falcao.
BOFYA PLAY HAPA CHINI KUCHECK MAGAORI HAYO
No comments:
Post a Comment