Mwili wa Adam Kuambiana ukipelekwa Hospitali ya Muhimbili.
KWELI kifo hakina huruma! Msemo huu umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana (38) kilichotokea akiwa njiani kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.Kuambiana aliugua ghafla kwenye kambi ya kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar.
NINI CHANZO CHA KIFO?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Jumamosi iliyopita nje ya Hospitali ya Mama Ngoma, msanii wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ alisema muda mchache kabla ya kufikwa na mauti, Kuambiana alimlalamikia maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa akiendesha damu tupu.soma zaidi>>>>>
No comments:
Post a Comment