06 February 2014

WILLIAM MALECELA "SIMCHUKII LOWASSA ILA SIMUUNGI MKONO NA MBIO ZAKE ZA URAIS"

 Baada tu ya Mh. Lowassa kutangaza ndoto yake kwenye Sherehe za Mwaka Mpya huko jimboni kwake, kukaaanza malumbano yakiongozwa na watu wake wa karibu sana wa kwanza alikuwa Msindai, Mgeja, Guninita, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar na Mwenyekiti wa CCJ chama kilichokufa kabla hakijaanza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha. Hawa ndio kweli Mh. Lowassa anayetaka Urais wa Jamhuri hii ndio aliowaona credible Leaders wa kumzungumzia kwa huu umma na kama sikosei kwa maneno mengine anatuambia kwamba akishika Urais wa Jamhuri hii hawa ndio tuwategemee kama Viongozi wakuu wa Taifa.

- Msindai aligombea Ubunge akashindwa, Mgeja chini ya uongozi wake Mkoa wa Shinyanga CCM imepoteza viti vingi vya ubunge kuliko mikoa yote huku Bara, Guninita amegombea Uenyekiti wa Mkoa wa Dar akashindwa na chini ya uongozi wake Majimbo mawili muhimu sana yameenda Upinzani, lakini kweli Lowassa anaamini kwamba hawa wanaweza kumsaidia kuifikia ndoto yake hiyo ya muda mrefu sana kama alivyosema mwenyewe.

- Well, simchukii wala simuungi mkono na mbio zake, lakini kwa hayo machache niliyokwisha yaona na kuyasikia maana yake ni moja kwamba sitapata shida ya kuamua kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa kuamua mgombea ambao mimi ni mjumbe kama nimpe kura yangu au hapana, iwapo jina lake litkuwepo!!

- MAKALA YANGU NZIMA YA HII HABARI ITAKUWA KWENYE GAZETI LA JAMBO LEO JUMAPILI.

Le Mutuz

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname