Na Gladness Mallya
WIMBI la wasanii kuingia
kwenye siasa limeendelea kushika kasi ambapo awamu hii msanii wa maigizo
na filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ametangaza kugombea ubunge kwenye
uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
‘Akistorisha’ na paparazi wetu, Dude alisema kutokana na sanaa
kutotoa masilahi ipasavyo, ameamua kuingia kwenye ulingo wa siasa ambapo
anatarajia ‘kunyakua’ Jimbo la Tabora Mjini ambalo kwa sasa linaongozwa
na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage.
“Natarajia kugombea ubunge nyumbani kwetu Tabora mjini, niko tayari
kuchuana na Rage na kwa sasa nipo katika maandalizi ikiwemo kuwa karibu
na wananchi kwani wananikubali sana, hivyo natarajia ushindi tu,”
alisema Dude.
No comments:
Post a Comment