07 February 2014

NI KWELI WAGANGA WANAFANYA NYOTA ZA HAWA WASANII 3 KUNG’AA?

Imekua kama story fulani,unaweza kusema ni fununu kwa baadhi ya wasanii wanao-hit kusemekana kuwa mbali na juhudi zao na kazi zao nzuri, ndani yake kuna mkono wa mganga flani hivi aliyeweza ku-boost mafanikio yao,na hata baadhi yao waganga kuibuka na kudai kuwa wao huwa ndio kimbilio la kwanza pale msanii awapo na shida ya kutaka kutoka kimuziki,hapa ugumu unakuja ni pale mtu unapokuja kujiuliza,yupi haswa wa kuamini either ni mganga anayedai kuwa yeye ndio chanzo cha mafanikio au ni msanii mwenyewe anayedai kuwa ni kazi tu ya mtu ndio itakayomfanya aweze ku-shine.
AT
AT msanii maarufu sana kwa staili ya miondoko ya mduara hivi maarufu sana hapa town,nae yalimkuta haya mambo ya waganga,kutokea mganga mmoja akiwa  anadai kua anamuomba ammalizie deni lake baada ya kazi yake kukamilika na kusababisha mafaniko makubwa ya msanii huyu hadi kufikia ku-make headlines na kupata show mbalimbali za nje ya nchi,mganga huyo maarufu kama Dk Shaarifa aliyasema haya:
Dk Sharifaa (Mganga)
‘‘Tangu bado hajafahamika yaani sio mwanamuziki mimi nilikutana naye Zanzibar Unguja,tena nakumbuka kwa mara ya mwisho alikuja na Gelly  wa Rhymes lakini Gllry alikuwa afahamu kitu chochote, chakushangaza tangu nilipomfanikishia mahitaji yake maana mimi ni mganga basi amenisahau kabisa nikijaribu kumpigia simu hapokei mpaka anapokea tuzo , anapata safari za kwenda muscat amenisahau mimi ninaomba anipatie vile vitu alivyoahidi kwangu anipatie,sio kwa ugomvi ila sheria zetu sisi waganga kwasababu hizi ni kazi namdai deni la laki tisa nikimpigia simu hapokei ndio maana nimekuja hapa kuripoti’
Alisema Mganga huyo.
‘Vitu vingine nilivyomsaidia vipo vingi kwa mfano anapotarajia kuachia wimbo mpya basi anakuja na Cd kwangu na mimi nafanyia taaluma yangu ya Uganga mwisho wa siku unakuta nyimbo zake nyingi zinapamba.Mimi naitwa Doctor Shariffa
fb3cc30684e411e380840e640719c695_8
Diamond Platnumz nae yalimkuta haya  haya mambo na kusemekana kuwa kuna mganga ambaye anafanikisha ku-hit kwake ,inasemekana kuwa sababu ya diamond kuja ghafla katika game na kuhit kwa haraka na kuzidi kupata mafanikio na utajiri mkubwa inasemekana naye alikuwa na mganga aliyekuwa nyuma ya mafanikio yake na sio kazi peke yake kama anavyodai platnumz mwenyewe,sidhani kama ni wote wanaoweza kuamini kuwa uganga unasaidia ila kwa wanaoamini inasemekana kuwa inawezekana kuwa yasemwayo yapo.
rich_mavoko
Rich Mavoko baada yaku-hit na nyimbo zake kadhaa,baada tu ya diamond kuanza ku-hit ikasemekana kuwa naye anamkono wa mganga nyuma ya mafanikio ya nyimbo zake,na cha zaidi ilisemekana kuwa mganga wa Diamond na wa avoko hawapatani kabisa na ndio sababu hadi hivi leo hakuna collabo ya wawili hawa,ingawa nyimbo zao wote wawili ndizo zinazoongoza kupewa airtime katika media mbali mbali hapa town

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname