Mahakama moja nchini Spain kwa
sasa inafanya uchunguzi kuangalia kama kuna mchezo wowte mchafu
ulifanyika katika uhamisho huo, wakati tayari Sandro Rosell
ameshajiuzulu kama raisi wa Barca mwezi uliopita kutokana na sakata
hili.
A
Uhamisho wa Neymar unachunguzwa nchini Brazil,
huku klabu ya zamani ya Neymar Santos na taasisi ya uwezekezaji ya DIS
Esporte wakisema wanahitaji kulipwa zaidi kutokana na dili hilo.
Wote
Neymar Snr na Barca wanasisitiza hakuna kitu chochote kilichoenda
kinyume kisheria wakati wa uhamisho huo, huku Barca wakichukua hatua
nyingine kuelezea malipo ya 40
million euros waliyolipa kampuni ya N&N -- inayomilikiwa na wazazi
wa Neymar --- 2.7 million euros alilipwa Neymar Snr kama kamisheni, pia
kuna malipo mengine ya makubaliano ya kibiashara na taasisi inayodili na
mchezaji, yote ambayo yanafikia jumla ya 8.5 million euros.
Leo hii Neymar alitumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuandika ujumbe ufuatao kuhusu uhamisho wake.
"Niliamua
kufunga mdomo wangu mpaka hivi sasa, lakini siwezi kuendelea tena,
kusikiliza ujinga unaozungumziwa kuhusu uhamisho wangu. Nilimpigia simu
baba yangu nikamwambia nataka nizungumze kuhusu suala hili, lakini
alinikataza na kuaniambia nikae kimya na kuweka umakini katika
kujiangalia vizuri ili niweze kupona haraka, akisema hili suala lilikuwa
likimhusu yeye.
Lakini
atanielewa kwanini nafanya hivi. Niliwaomba watu ninaofanya nao kazi
wanisaidie kuandika. Nisamehe baba kwa kutokukusikiliza kwa mara ya kwanza, lakini nitaongea.
"Napenda
kukushukuru kwa namna ulivyoweza kushughulikia maisha yangu ya soka,
biashara ulizozitengeneza kuzunguka kazi yangu na namna ulivyoweza
kuitunza familia yetu.
Kama niliichezea klabu iliyopo moyoni mwangu Santos na leo naitumikia
klabu ya ndoto zangu Barcelona - yote hii shukrani zije kwako.
"Nafahamu
watu wengi wanaongea ujinga kutuhusu, hata kuwa na mashaka na maadili
yetu.....vilevile nimegundua kiasi cha marafiki wanafki
tulionao....Baba, wakati Thiago Silva aliposema atakufa kwa ajili yangu
uwanjani, na mimi pia nilikuwa tayari kumfanyai hivyo yeye. Lakini kwako
wewe baba, sitokuwa tayari kufa mimi tu bali nitayatoa maisha hata ya mwanangu kwa ajili yako!
"Kwa
hili nakuomba.....rudi Hispania, nakukumbuka. Siku chache zijazo
nitarudi kucheza na nakuhitaji uwe hapa. Muda utaonyesha hujafanya kosa
lolote. Kwamba ulikuwa tu bi baba bora kwangu. Nakupenda." Chanzo: shaffihdauda
No comments:
Post a Comment