Naitwa
Dada Tunu, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 33,nipo kwenye
wakati mgumu sana katika maisha yangu, najitokeza kwenu
watanzania wenzangu ili mnishauri nifanye nini. Kwa ufupi ni
kwamba, niliolewa mwaka 2001,kisha mimi na mume wangu tukahamia
Morogoro. Sikubahatika kupata mtoto hadi mwaka 2010 ambapo
nilijifungua mtoto wa kike, hata hivyo mtoto huyo hakuwa riziki
kwani miaka miwili baadaye alifariki dunia, hii ilikuwa mwezi
Machi 2012, niliumizwa sana na kifo hicho, ukichukulia manyanyaso
niliyokuwa nayapata kwa mawifi zangu, wakwe zangu na mume wangu
mwenyewe kutokana na kutobeba ujauzito, miezi mitatu baadaye mume
wangu alinifukuza na kuoa mwanamke mwingine. Siwezi kuelezea
uchungu nilioupata. Nilifukuzwa kama mbwa. Nilifikia hatua ya
kutamani hata kujiua lakini
Mungu
aliniepusha. Baada ya tukio hili niliamua kurudi nyumbani kwa
wazazi wangu. Nikiwa nimesharudi nyumbani kwetu, siku moja
nilikutana na dada mmoja ambaye alikuwa rafiki yangu wa tangu
utotoni, huyu na yeye alikuwa ameolewa na kuachika kwa mumewe,
aliachwa na watoto watatu, wa kwanza alikuwa na miaka 7.
Nilishangaa kumuona rafiki yangu huyu akiwa na mafanikio makubwa
sana. Alikuwa na majumba, magari na biashara mbalimbali .
Nilijiuliza maswali mengi sana, kuhusu mahali alipo upata utajiri
wake kwani nakumbuka ni miaka miwili tu iliyokuwa imepita
nilipokuwa nimerudi kutembea nyumbani nilikutana naye akiwa na
maisha magumu sana, alikuwa ndio ametoka kuachwa na mume wake .
Baada ya kuongea naye kwa kirefu nikimuomba anisaidie na mimi
niwe kama yeye, aliamua kunipeleka kwenye kikundi chao. Kikundi
hiki ni cha wanawake walio achwa na waume zao. Dada huyu
aliniunganisha kwa mkuu wa hicho kikundi ambaye wao walikuwa
wanaumita DADA MKUBWA ama BIG SISTER. Dada mkubwa alinihoji
maswali mengi sana, baadaye akaniambia nirejee baada ya siku
saba, baada ya siku saba, akakichukua na kunipeleka kwenye
hoteli moja ya kifahari hapa hapa jijini Dar Es salaam. Huko
nilikutanishwa na wanawake wenzangu kama kumi na mbili ambao
nao walikuwa wamepelekwa kwa mara ya kwanza. Baada ya kupewa
maelekezo, tulipelekwa kwenye chumba maalumu ambapo tulinganishwa
na wanawake wengine kama thelathini ambao ni matajiri sana,
baadhi yao niliwatambua kwa sura kutokana na umaarufu wao.
Wengine ni wake za watu, watu maarufu, wanafunzi wa vyuo na
sekondari na wengine ni raia wa nchi nyingine kama vile Nigeria,
Ghana na Kenya. Wote hawa walikuwa wamevaa mavazi maalumu.
Tulipewa maelekezo maalumu ambapo baadaye wote tulitakiwa kuvua
nguo zetu na kubaki kama tulivyo zaliwa. Ibada ilio ongozwa na
wanaume watatu walio valia mavazi maalumu, kiongozi wa ibada
alikuwa mwanaume kijana mdogo tu ambaye wakati wote alikuwa
anazungumza maneno nisiyo yaelewa. Baada ya hapo ikawa kila
wiki tunarudi tena kufanya ibada hii na kila wiki kulikuwa na
wanawake wapya zaidi ya ishirini ambao wameletwa kujiunga. Hapa
ndio nikawa nimeingia rasmi kwenye kanisa hili la kusali uchi
bila kutarajia Miezi sita baadaye nikawa tayari namiliki nyumba
kadhaa, magari na biashara zinazo nilipa sana. Ingawa katika
kanisa hili hakuna masharti ya kutoa damu za watu, lakini
ukiingia katika kanisa hili unafanya mkataba maalumu na shetani,
kwanza utatakiwa kumtumikia shetani katika maisha yako yote ya
hapa duniani ambayo maana yake ni kwamba, unakuwa umekubali
kuwa na maisha mazuri hapa duniani na utakapo kufa uende
jehanamu. Utapata kila kitu unacho kitu unacho kitaka, kuanzia,
pesa, magari,majumba,mapenzi, nguvu, exposure na kila kitu kizuri
unacho kijua wewe, lakini kwa sharti la kuuza roho yako kwa
shetani. Ukiingia kwenye kanisa hili ni hakuna kutoka, wala kutoa
siri zao. Ukitoka utapata matatizo makubwa na ukijitoa ndio
balaa. Mimi nimeamua kujitoa mhanga ili kuwasaidia watanzania
wenzangu hasa wanawake kwa sababu kuna wanawake wengi sana
kuanzia wanafunzi wa shule za sekondari, vyuo, wake za watu ,
wafanyakazi ,wafanyabiashara hadi watu maarufu wamekuwa wakijiunga
na kanisa hili kila kukicha kwa ajili ya kupata huo utajiri
wa kishetani. Sikushauri ufanye hivyo kwani mwisho wa siku nafsi
yako itaangamia. Binafsi ninaumia sana moyoni kuona kuwa nina
mali, na utajiri mkubwa lakini nimeupata kwa shetani na siku
nitakayo kufa ninakwenda Jehanamu. Sina raha na utajiri wangu na
ninatamani niyatelekeze majumba yangu, kisha niende nikaishi
maisha yangu ya awali, ya kimasikini lakini nikiwa na amani
moyoni, ila ninashindwa kwa sababu nilisha jifunga na kanisa
hili.
Ninaomba ushauri wenu watanzania wenzangu, ninataka
kujitoa lakini ninaogopa madhara ninayo weza kuyapata kutokana na
kujitoa. Nifanye nini ili niweze kujitoa. . Unaweza kuniandikia
kupitia barua pepe yangu : tunukondo@gmail.com
Tueleze vizuri ukiingia hapo au ulipoingia hapo utajiri ulikujeje?Je, ulipewa magari na mapesa na hayo majumba ukaanza kuyamiliki?Huyo shetani mnaongea naye wapi na kivipi kama siyo watu wenyewe au kuna kitu kingine mnafanyiwa hujatueleza?Hao wanaume wanaoongoza ibada za kishetani huwaambia nini hasa.Na uchi wenu huo mnaowaonyesha kwenye ibada hizo wanaufanyia nini hao wanaume watatu wanaoongoza ibada zenu?
ReplyDelete