Mwigizaji wa kike mwenye mvuto katika tasnia ya filamu Bongo yupo katika mapumziko ya uzazi baada kuamua kuachana na kila kitu ili apumzike kwa ajili ya kulea mimba yake ambayo ni kubwa na anatarajia kujifungua hivi karibuni na anasema amechoka kutokana na hali hiyo hana hata muda wa kujiremba tena.“Nimechoka sana hapa nilipo sihitaji kujiremba wala kitu chochote kinachohusu urembo, nipo tu nahitaji kupumzika kwa ajili ya afya yangu na ya mtoto wangu, urembo kwa sasa nimewaachia warembo wajipodoe na muda ukiruhusu nitarejea katika urembo tena,”anasema Odama.
Mwigizaji huyo ambaye ni mtayarishaji wa filamu pia kwa sasa amesimama hata kazi zake za kurekodi au kuandaa sinema kwa ajili ya ujauzito ambao kwake imekuwa ni kazi nyingine nzito na mwenyewe anasema anajali afya yake kwanza na kusubiri wakati ufike akijifungua na kurudi katika hali yake ya kawaida ataendelea na utengenezaji wa filamu kama kawaida.
No comments:
Post a Comment