Mwanamke huyo pichani anayeitwa Belinda
mwenye umri wa miaka 32, akiwa na mume wake wa kwanza, Yasemekana
mwanamke huyu alifanikiwa kufanya udanganyifu huo kwa kushirikiana na
Baba yake mzazi.Gazeti la The Finder nchini Ghana liliripoti kuwa
mwanamke mwanamke huyo aliolewa na mume wake wa kwanza Maxmus Anumah
ambaye ni mfanyakazi wa Hospitali ya kijeshi ya 37 mwaka 2012 kisha
kuolewa na mwanamume mwingine Audrey Atikpo January 2013 huku akiwa
bado katika ndoa ya awali.
Ilielezwa kuwa katikati ya january 2013,
Belinda ambaye alionyesha kutofurahishwa na ndoa baina yake na mumewe
wa kwanza, alimuomba ruhusa mumewe huyo ya kwenda kwenye kituo cha
maombi cha Edumfa kwaajili ya sala ya kufunga ili wapate watoto, ambapo
mumewe alikubali ombi hilo.
Huku mumewe akiwa hajui kinachoendelea,
Belinda kwa kushirikiana na Baba yake na baadhi ya wanafamilia waliandaa
ndoa ya siri ya binti huyo kwa mwanamume mwingine Audrey Atiko ambaye
alikuwa amerejea kutoka Marekani na haijafahamika kama waliwahi kukutana
awali au la.
Ripoti hiyo ilieleza pia kwa mujibu wa
vyeti vya ndoa yake ya pili.Belinda aliolewa na Atikpo January 31,2013
na waliandikisha ndoa hiyo kwenye mahakama ya wilaya ya Somanya.Baadaye
jamaa huyu alikodi nyumba ya makazi kwenye eneo lijulikanalo kama East
Legon ambapo aliishi na Belinda kwa muda mfupi kisha kurejea Marekani
kwaajili ya kuandaa utaratibu wa kumuwezesha Belinda kuungana naye kwa
kwenda nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo baada ya
Atikpo kuondoka Belinda alikusanya vitu vyake na kurejea kwa mumewe wa
kwanza katikati ya mwezi wa pili, 2013.Ilielezwa baada ya kurejea huko
Belinda alianza kukosoa kila alichokuwa anafanya mume wake huyo wa
kwanza na kusababisha mzozo ya kila mara baina yao.
Miezi kadhaa baadaye, baba yake
alikwenda kuwatembelea na kusema kuwa Belinda anahitaji apewe talaka,
lakini mume wake huyo alikataa kufanya hivyo, Baada ya kupata shaka
kuhusu simu za mara kwa mara kwa mkewe kutoka kwa watu tofauti ambazo
alibaini zinapigwa kutoka Marekani, Maximus alihitaji kupata maelezo
kuhusu simu hizo na Belinda alimwambia kwamba mwanamume ambaye amekuwa
akimpigia simu (yaani mumewe wa pili, Atikpo) ni binamu yake na mwanamke
ambaye amekuwa akiwasiliana naye (yaani mama mkwe wake aliyeko
Marekani) ni shangazi yake.
Kwakuwa hakuridhika na majibu, Maximus
aliamua kuanza kumfuatilia kimya kimya na katika juhudi hizo alibaini
kipande cha karatasi, kilichokuwa chumbani kwao kikiwa na jina na
anauani ya Atikpo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jamaa aliamua
kutumia mtandao wa facebook kutafuta jina la Audrey Atikpo kisha
kumtumia ombi la kuomba urafiki. Baada ya kukubali ombi hilo na kisha
kuona picha ya harusi ya Belinda na mume wake wa kwanza kwenye ukurasa
wa facebook, Atikpo alianza kumshambulia Maximus kwa ujumbe mkali ambaye
kila mmoja alieleza kwamba ndiye mume halali wa Belinda.
Kwa mujibu wa The finder, siku
iliyofuata Atikpo alimpigia simu Belinda kutokea Marekani na kumuuliza
kuhusu suala hili, ambapo Belinda aliamua kukusanya kila kilicho chake
kutoka nyumbani kwa mume wake wa kwanza na kwenda kwenye nyumba
aliyokuwa amepangiwa na Atikpo. MMMH YAANI HILI NI BALAA, AIBU GANI HII
CHANZO. MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment