MAISHA yanahitaji kitu gani tena? Ukiwa na akili na ukiitumia
vizuri akili yako, utapiga bao la maisha. Hiki ndicho alichokifanya
straika Mtanzania, Danny David Mrwanda. Ndio maana marafiki zake huwa
wanamtania kwa kusema kuna ‘Mrwanda mmoja tu duniani.’
Si kosa kusema, Mrwanda ni milionea, kutokana n
a utajiri alionao anaweza kuishi maisha yoyote anayotaka bila hata kucheza soka. Kazi yake ni soka, fedha anazopata kutokana na soka kama usajili, mshahara na posho aliwekeza na sasa ukimtaja Mrwanda unamzungumzia mwanasoka mwenye mali za maana.
a utajiri alionao anaweza kuishi maisha yoyote anayotaka bila hata kucheza soka. Kazi yake ni soka, fedha anazopata kutokana na soka kama usajili, mshahara na posho aliwekeza na sasa ukimtaja Mrwanda unamzungumzia mwanasoka mwenye mali za maana.
Anaweza kuingiza zaidi ya Sh350,000 za Kitanzania
kwa siku sawa na Sh15 milioni kwa mwezi, kupitia vitega uchumi vyake vya
biashara anazomiliki Tanzania.
Mrwanda alishtuka mapema na kupanga mambo yake,
alitunza pesa na kufanya mambo ya maendeleo akiogopa kuumbuka baada ya
kustaafu soka kama inavyotokea kwa wachezaji wengi.
Mrwanda anasema: “Kama mchezaji, nimejifunza
kutokana na mazingira kupitia maisha wanayoishi wachezaji wengine
waliotutangulia, nikakuna kichwa, nikajipanga.”
Utajiri wake
Maisha anayoishi Mrwanda jijini Dar es Salaam
anastahili kuitwa staa na profesheno wa ukweli. Anamiliki nyumba kubwa
ya kisasa iliyopo Kisukuru, Tabata, Dar es Salaam. Kwa haraka makadirio
ya thamani ya mjengo huo ni Sh 200 milioni.
Anamiliki usafiri wa nguvu aina ya Nissan Murano,
gharama yake ni kama Sh60 milioni. Mbali na hivyo, anavyo viwanja vinne
vyote viko jijini Dar es Salaam kati ya hivyo viwili ameshaanza kujenga
na shamba la ekari moja lililopo King’azi, Kinyerezi, Dar s Salaam.
“Mpango wangu ni kujenga nyumba za biashara kama
hapa (anaonyesha kiwanja kimoja ambacho kipo karibu na nyumba anayoishi
hapo Kisukuru), unaona nimeanza kujenga fremu za duka kwanza huku, kule
kwingine naangalia kwanza, naweza kujenga nyumba ya kulala wageni au
kupangisha.
“Lile shamba kule bado nalima mazao mbalimbali na
kufuga tu, ila nina mpango mkubwa hapo baadaye kwa sasa naangalia kwanza
upepo ili nifahamu niweke kitu gani kitakachoniingizia kipato,” anasema
Mrwanda.
Mbali na ardhi, ukikutana na daladala yoyote kwa
nyuma imeandikwa ‘Mrwanda The Straika’ kwa chini ‘Maximo’ na mbele
‘Royal Prince’ usijiulize mara mbili kutaka kujua ni za nani? Ni mali
ya Mrwanda.
Mrwanda ndiye mmiliki wa daladala hizo, anazo nne,
mbili zinafanya safari za Mwenge-Kariakoo na nyingine Mwenge-Posta.
Kila daladala moja, inapeleka hesabu ya Sh85,000 kwa siku, ukizidisha
mara nne idadi ya daladala hizo ni Sh340,000 kwa siku
No comments:
Post a Comment