12 February 2014

ANGALIA PICHA ZA MSANII WA BONGO MOVIE APATA AJALI, ALAZWA

Tito Zimbwe' Actor Bongo Movie's Tanzania 
MSANII huyu maarufu na mkongwe katika tasnia ya filamu hapa nchini ambaye wengi walianzia kumtambua pale Kaole katika Tamthilia zilizotikisa Tanzania na vitongoji vyake..Nguli huyo wa filamu alifunguka kuwa ajali hiyo ilitokea mnamo siku ya Ijumaa 7/FEB/2014 usiku majira ya saa tano na nusu. Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni tuta lililowekwa barabarani bila alama yeyote au kiashiria cha kuonyesha kuwa eneo hilo kuna tuta kwahio dereva upunguze mwendo. Alikuwa akitokea kigogo sambusa kuelekea kinondoni kufika maeneo ya kigogo lutihinda mkabala na Shule ya Msingi Lutihinda Primary School alishangaa ghafla amedunda kwenye tuta na kupaa hewani kutua chini akashindwa kuizuia pikipiki ikamgaragaza kwa bahati nzuri mungu mkubwa kwakweli aliumia lakini hakuvunjika popote zaidi ya kuchubuka mikononi na miguuni. 
Maranyingi msanii huyo hutumia gari lakini sikuhio aliamua kutoka na pikipiki kumfuata rafiki yake mpendwa Beni Branco mzee wa Vituko Vituko aliyekuwa swaiba sana wa marehemu Steven Kanumba, Ajali hiyo ikawa mwisho wa safari ya kwenda kumsalimu Beni Branco.  
Mpaka sasa 'Tito Zimbwe' yupo Kinondoni katika Hospitali ya Private ya Doctor Mvungi. Anaendelea na matibabu, Hali yake ni nzuri kwa mujibu wa yeye

mwenyewe...
Shemejietu (Mkewe) kushoto akimliwaza kaka Tito Zimbwe 
usijali shemeji mzee atapona sisi ndugu zakeZINAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname