Duniani kote inapofika mwishoni mwa mwaka, jamii hujumuika makanisani, misikitini,kwenye kumbi za starehe, majumbani japo kutoa shukrani zao kwa mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kuuona mwaka mpya.....
Katika
kuusindikiza mwaka ulioisha 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa
2014, aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Lowassa naye aliamua
kujumuika na wageni katika sherehe aliyoiandaa jimboni kwake
Monduli...
Ikumbukwe
kwamba, inapofika saa saba kamili usiku wa kuamkia mwaka
mpya,hoihoi, vifijo na shamrashamra vinasikika kwa staili
tofauti;wengine wakirusha fataki hewani,wengine wakipiga debe,meli
zikipiga honi,bendi kwenye kumbi za starehe zikipiga nyimbo za
kuukaribisha mwaka mpya ilihali yote yakiashiria kufurahia ujio
wa mwaka mpya.Mara nyingi, viongozi mbalimbali hupata nafasi ya
kutoa salamu za mwaka mpya...
Waziri
mkuu mstaafu, Lowassa, katika sherehe hizo aliyoiandaa jimboni
kwake Monduli ya kuuaga mwaka 2013, mbele ya wageni wakati
akitoa salamu ya kuukaribisha mwaka mpya alinukuliwa akisema
"Anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto za
watanzania ya kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya
uhakika"
Hata
hivyo, kwa mshangao wa walio wengi,baadhi ya watendaji wa juu
wa CCM na baadhi ya watendaji kutoka UVCCM taifa walijitokeza
hadharani kubeza kauli hiyo ya Lowassa utadhani aliyoyatamka
yalilenga kudhoofisha nguvu ya chama hata kuitumbukiza nchi
kwenye mifarakano
Mmoja
wa watendaji wa UVCCM aliyejitokeza kumrushia madongo Lowassa
ni katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi taifa, Paul
Makonda. Bila kutaja jina la mtu lakini akitafsiriwa kumlenga
moja kwa moja Lowassa alisema, nanukuu: "Watu wanatangaza kutoa
elimu bora, kwa nini wasifanye hayo kupitia chama?"
Alienda
mbali kwa kudai kwamba:"Kamati ya maadili CCM inayoongozwa na
Mangula ilipaswa kuonesha wazi hasira zake kwa vitendo". Maneno
haya kutoka kwa kiongozi huyo wa chipukizi siyo tu kwamba
yanachefua,bali yanaonyesha dhahiri kukosekana kwa mafunzo ya
awali ya itikadi na sera ya chama kwa makada hawa chipukizi.
Kuna
mambo kadha wa kadha yanayoitesa CCM na jumuiya zake japo
wanajifanya hawayaoni.Tatizo kubwa ni kwamba makada wengi
wameambukizwa gonjwa hatari la kujipendekeza kwa wakubwa
ilimradi kukamilisha msemo usemao:"Funika kombe mwanaharamu
apite".
Hakika
gonjwa hili la unafiki,ubinafsi na kujikweza kwa sasa limeenea
na linatafuna vyama vyote vya siasa hapa nchini na siyo CCM
pekee.Sioni mantiki kwa Makonda, Nape Nnauye na wengine wa namna
yao kushupalia kauli ya Lowassa ilihali wakijua wazi pasipo
shaka kwamba mbunge huyo wa Monduli ni mjumbe halali wa
halmashauri kuu ya taifa na mojawapo ya majukumu yake kama
mjumbe ni kuendeleza sera na ilani ya CCM kwa vitendo....
Kauli
ya Lowassa haikutofautiana na majukumu halisi yaliyoainishwa
kwenye ilani ya uchaguzi wa CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu
wa mwaka 2010 kwa kuzingatia dira na maendeleo ya taifa 2025
na malengo ya Millennia.
Kwa
faida ya wasomaji, napenda kunukuu sehemu hiyo ya Ilani
inayosomkea: "Katika kipindi cha ilani hii 2010 - 2015, mchakato
wa kujenga uchumi wa kisasa utatekelezwa katika maeneo
yafuatayo:
"Kuimarisha
na kuboresha elimu, kuandaa rasilimali watu katika maarifa na
mwelekeo, kufanya mapinduzi ya kilimo, kufanya mapinduzi ya
viwanda na mengineyo mengi"....
Kwa
kuwa sera ya CCM ni kutaka kuwaletea wananchi elimu bora, na
kwa kuwa falsafa ya Rais Kikwete ni kutaka kuwaletea wananchi
maisha bora kwa kila mtanzania, na kwa kuwa sera ya CCM
ndiyo dira ya maendeleo ya taifa 2025, swali la kujiuliza, Je,
Lowassa alikosea nini hadi Makonda na wenzake wakashupalia kwa
maneno makali eti kamati ya maadili CCM ilipaswa kuonyesha
wazi hasira zake kwa vitendo?
Kati
ya Lowassa na Makonda, ni nani alipaswa kuonyeshwa hasira na
kamati ya maadili kwa vitendo? Nasema bila kumung'unya maneno
kwamba ukosefu wa mafunzo ya maadili ya chama yaliyokuwa
yakitolewa tangu enzi za TANU,CCM hadi 1972 hakika umeleta
madhara makubwa kwa makada wapya ndani ya CCM na jumuiya
zake...
Kumjengea
Lowassa na wenzake wa aina yake mazingira ya vitisho ni sawa
na kumsafishia njia kwa kupitia mlango wa nyuma....
Kuna
baadhi ya makada ambao bado wanaota enzi za chama kimoja
kushika hatamu ambapo wanachama walitishiwa kutothubutu kusogelea
nafasi za juu bila idhini ya wafalme ambao siku zote
walifikiria kuwarithisha familia nafasi hizo....
Haiingii
akilini kwamba makada hawa chipukizi ambao hata itikadi na
mwongozo wa chama hawavijui, eti nao wanadiriki kumkemea mjumbe
wa halmashauri kuu hususani mtu kama Lowassa abaye ni kada
aliyebobea na anakifahamu chama kulikoni huyo Makonda wa kuja
ambaye ni mpya kwenye chama...
Uongozi
ni kipaji na kamwe kipaji cha mtu hakiwezi kuzuiliwa kwa
staili kama hii ya kelele za chura ambayo haimzuu ng'ombe
kunywa maji....
Sina
nia wala sikusudii kumfagilia Lowassa, lakini inapaswa kueleweka
kwamba Lowassa hajitangazi mwenyewe wala hajipitishi kama wengi
wanavyomfikiria.Bali anatafutwa na viongozi mbalimbali kutoka
taasisi za kijamii na kidini kwenda kuimarisha taasisi hizo...
Wenzetu
wa nchi jirani ya Kenya, wao walianza siku nyingi kuchangia
taasisi za kijamii kwa staili ya harambee.Hata kwenye nembo ya
kitaifa inaonyesha harambee ikiwa ni ishara ya kuisaidia
jamii.Siyo vibaya hata sisi hapa kwetu tukaiga jambo hili jema
na ikawa ni sehemu ya utamaduni wetu katika kuisaidia jamii
yenye matatizo....
Serikali
haiwezi kuwafikia wananchi wake kila kona.Aidha serikali
haiwezi kuwatimizia wananchi mahitaji yao yote pasipo
kuwahusisha wananchi na viongozi kwa staili ya harambee...
Ushauri
wangu ni kwamba;watendaji wakuu wa chama na jumuiya zake,
wapime kwanza uzito wa kauli zao kabla hawajazitoa mbele ya
jamii.Watumie busara zaidi katika kuwaunganisha wanachama
wao.Kurushiana makombora katika muda huu mfupi uliobaki
haitawasiadia...
Kitendo
cha kuendelea kumshupalia Lowassa kama vile ni msaliti wa
chama kinakipunguzia chama haiba na mvuto mbele ya jamii...
Mwacheni
Lowassa na watu wa aina yake wakitumikie chama badala ya
kutikiswa kila mara huku wakitekeleza sera za chama....
Kama
Mungu alimpangia Lowassa nafasi au hata maisha flani ya juu
kiuongozi, hakuna yeyote mwenye ubavu wa kumzuia...
Uongozi
unahitaji hekima na busara na si vinginevyo. Mwacheni Lowassa
kwa kuwa anaijua vema CCM kulikoni hawa wakuja...
>>Kwa hisani ya: Tazama Tanzania
No comments:
Post a Comment