Kwa muda mrefu Tanzania jina la mfanya
biashara maarufu, Chifu Kiumbe limekuwa intro ama outro kwenye nyimbo
nyingi za wasanii wa bongo flava na muziki wa dansi nchini kutokana na
misaada mbalimbali anayoitoa kwa wasanii hao.
Maswali mengi yamekuwa yakiulizwa kwa
muda mrefu bila majibu sahihi kutoka kwa mhusika mwenyewe ‘kwa nini
hutoa misaada hiyo na yeye anafaidika na nini?
Chief Kiumbe ambaye jina lake halisi ni
Muhammed Abdallah Kiumbe, amefunguka exclusively kupitia kipindi cha Sun
Rise cha 100.5 Times Fm katika ‘Exclusive Friday’ ikiwa ni kwa mara ya
kwanza kwake kufanya mahojiano na kituo cha radio hapa nchini.
Akifanya mahojiano na Samira, Fadhili
Haule na Erick, Chifu Kiumbe aliweka wazi kuwa yeye ndiye aliyemnunulia
Diamond Platinumz gari aina ya Toyota Land Cruiser V8. Na kwamba
alilinunua kwa $100,000 na ushuru alilipia takribani Million 85 za
Tanzania.
“Kuna rafiki yangu hapa mmoja magazeti
yanamuandika andika yanasema ‘mzee wa kuloga, japokuwa…rafiki yangu
Diamond. Naseeb ni rafiki yangu, swaiba wangu na kipenzi changu. Kuna
gari moja kubwa sana analitembelea sasa hivi, zuri sana…najua mnajua
lakini mnataka tu nizungumze.” Chief Kiumbe amefunguka kwenye kipindi
cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm.
“Ni gari ya thamani, kwa sababu
nafikiri…nililinunua $100,000 na ushuru wake kama million 85 (za
Tanzania), ukijumlisha inakuja kama ‘two forty five’, ni kama million
245.” Ameeleza.
Akielezea sababu za kumnunulia Diamond
gari hilo, amesisitiza kuwa ni rafiki yake wa karibu na kwamba kuna
mambo ya ndani wanayafahamu wao wawili kama marafiki, “aah..ni mshikaji
wangu Diamond, tumeongea naye kiundaniundani mimi na yeye.”
Alipoulizwa kama kuna mkataba wowote
kati yake na Diamond, Chief Kiumbe alifunguka, “hakuna
mkataba…nimekwambia ni rafiki yangu na swaiba wangu kwa hiyo tunayajua
wenyewe chini ya kapeti.”
Hata hivyo, amekiri kuwa Diamond ni
msanii mwenye pesa nyingi kwa kiwango chake na kwamba anafanya vizuri
kwenye muziki wake, na pia akawashauri wasanii wengine waige mfano wake
ili waweze kufanikiwa pia zaidi katika kazi zao za muziki kama
alivyofanya Diamond Platinumz.
Akizungumzia kuhusu kile anachokipata
kwa wasanii kufuatia misaada mbalimbali mikubwa anayowapa, amesema kuwa
yeye hutoa bure na hategemei kurudishiwa. Ametoa mfano kuwa kwa kipato
cha wasanii wa Tanzania hakuna ambacho watampa.
“Nadhani dada unaweza ukaelewa maana ya…
(akataja neno la kiarab lenye maana ya kutoa msaada) kutoa msaada bure.
Sasa ngoja nikuulize swali sawa, mfano mimi sawa, Diamond akipiga show
yake ama Tunda akipiga show yake sawa…sasa atanipa nini?” ameeleza.
Lakini hakuna kitu cha bure ‘there is no
free lunch in America’, Chief Kiumbe ama The Big Boss kama wanavyomuita
waasanii ameeleza kidogo anachokipata kutoka kwa wasanii hao.
“Yeye anakuja kwangu, shukurani kwangu
kwamba labda ‘swaiba wangu wewe una party’, nina birthday ya mtoto wangu
Halima, au mke wangu birthday yake mama Rajab. Kwa hiyo njoo Diamond
unipigie birthday yangu ya watoto wangu tufurahi hapa nyumbani. Basi
Tunda njoo ukamue hapa, Shetta njoo ukamue hapa.”
Mfanyabiashara huyo ambaye ameeleza kuwa
ni mmiliki wa bendi ya Extra Bongo lakini mafao yote anayachukua swaiba
wake Ally Choki ambaye amemtaja kama mtu aliyelitangaza kwa mara ya
kwanza jina lake Tanzania, amesema amewapa mkataba wasanii wote
wanaohusika na bendi ya Extra Bongo ambao unampa msanii nyumba na gari
ambavyo anavitumikia katika kipindi cha miaka mitano katika bendi hiyo.
Ameongeza kuwa, mbali na kuwasaidia
wasanii hujihusisha pia na kuisaidia jamii na kupitia huko hapendi
kujitangaza. Ametoa mfano kuwa aliisapoti kwa kiasi kikubwa ziara ya
Diamond alipotembelea vituo vya watoto yatima.
Kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm
huendeshwa na Samira, Fredwaa, Fadhili Haule na Eric kila siku za wiki
kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu kamili. Unaweza
kusikiliza online kupitia tovuti hii. Bofya sehemu iliyoandikwa
‘Listen’.
Sikiliza hapa kipande cha mahojiano
hayo, na endelea kutembelea www.timesfm.co.tz utamfahamu vizuri Chief
Kiumbe na biashara anazofanya na uhusiano wake na Raila Odinga wa Kenya.
No comments:
Post a Comment