11 January 2014

Licha ya Kutoswa na Diamond, Penny Afunguka na kusema "Naapa kwa Mungu wangu katika maisha yangu haitatokea kamwe nikamdharau Diamond, thamani yake kwangu itabaki palepale"

MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniel Mungilwa ambaye ni zilipendwa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ amesema katika maisha yake haitatokea akamdharau kwa kumkashifu hata kama si wake tena.

Akipiga stori na paparazi wetu, mwanadada huyo alisema japo kwa sasa ametofautiana na Diamond aliyeweka wazi kwamba yupo na Wema Sepetu hawezi kuwa na chuki dhidi yao. “Naapa kwa Mungu wangu katika maisha yangu haitatokea kamwe nikamdharau Diamond, haijalishi yupo na nani kwa sasa, thamani yake kwangu itabaki palepale hamuwezi jua namheshimu kiasi gani yule mtu,” alisema Penny.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname