Jacqueline Wolper akiwa na mchumba wake wa sasa G. Modo. |
17 January 2014
HUYU NDO MCHUMBA WA JACQUELINE WOLPER "GAMBE" !MCHEKI HAPA....!
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana
mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa
kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Wolper alisema alikuwa
kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kutafakari kwanza maana asingeweza
kukurupuka wakati bado hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake
huyo.
“Kiukweli nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja
kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na
Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi
niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment