17 January 2014

DUUU..MADEREVA BODABODA WAKIMBIA NA MAITI BAADA YA MCHUNGAJI KUWAAMBIA WAMEFUATA CHAKULA

Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.
 Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.
Kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole
Marehemu Gabriel Osward Ngalele. enzi za uhai wake
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani
Katikati mke wa Marehemu
Mwili wa marehemu ukiagwa makaburini hapo
Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname