Nay wa Mitego ametoa video mpya ‘Nakula Ujana’ wiki iliyopita ambayo
imefanyika nchini Kenya. Katika video hiyo Nay ameonekana akila ujana
haswaaa huku akiwa amezungukwa na mabinti wazuri watano wa Kenya,
waliojifunga taulo huku wakichezea kifua cha hit maker huyo wa ‘Muziki
gani’ ambacho kiko wazi.
Inavyoonekana video hiyo imeleta wivu kwa mpenzi wa Nay hasa kutokana
na jinsi alivyojiachia na warembo hao, hali iliyopelekea Nay atumie
Instagram kumtoa wasiwasi ‘mrs Nay’ juu ya wasichana hao walioonekana
naye kwenye video, hiki ndicho alichokiandika;
“Daaaaah!! #Nakula #ujana #video inataka kuharibu kwa bby… #966
ckiliza mrs nay hii ni video 2 hakuna kingine kilichoendelea baada ya
apo,,, ni kweli we ndo unastahili kushika icho kifua bt ni kazi 2 na
nikatika kufanya ki2 kizuri.. plzz tusigombane bcoz of zat zic video,,
sawa angeweza act m2 mwingine bt ckuona haja yakumuweka m2 nilitakiwa
kuonyesha uhalisia kidogo…@wemalious mi penda wewe sana kila m2 anajua,,
wale mabinti wa kikenya wackupe presure#966″.
No comments:
Post a Comment