08 January 2014
BARID KALI ILIYOPO MAREKANI NA U.K YAWAFANYA WABONGO WAISHIO HUKO WAJUTE KUISHI HUKO..NI FUL KUGANDA!!TAZAMA HAPA
Wakazi wa mashariki na kusini mwa Marekani wanapambana na baridi kali na ya hatari kuwahi kutokea baada ya dharuba ya upepo baridi kutoka maeneo ya kaskazini ya bara la Amerika kupiga na kuenea maeneo ya kati, kusini na mashariki ya nchi hii.
Hali ya baridi inayoweza kugandisha maji kuwa barafu na theluji katika muda wa sekunde chache imevunja rekodi ya baridi iliyotokea miaka 10 iliyopita na kufanya hali kuwa hatari kubaki nje na kusababisha maelfu ya shule na biashara kufungwa.
Kiwango cha baridi kimeshuka chini kwa nyuzi 10 chini ya sifuri kwenye kipimo cha Celsius hapa Washington DC , Philadelphia na Boston huku upepo ukiwa ni baridi zaidi na kufanya mtu kuhisi baridi kuwa chini ya kipmo hicho.
Kushuka sana kwa kiwango cha baridi kumesababisha kuahirishwa kwa maelfu ya safari za ndege na kuleta mtafaruku barabarani na kwenye njia za reli. Watabiri wa hali ya hewa wanasema karibu watu milioni 200 wanaweza kuathiriwa na hali hiyo.
Baadhi ya wahamiaji kutoka Afrika Mashariki wanasema hali hii inawasababisha kukumbuka nyumbani na hawajawahi kuona kitu kama hichi ambapo usipojitahadhari unaweza kuwa mgonjwa mara moja au hata kupoteza vidole vya mikono au miguu ikiwa hujavaa vizuri.
Hali hii ya baridi pia inafikia maeneo ya kusini ambayo ni nadra kupata baridi kama vile Florida na kusini mwa Texas kawaida maeneo hayo huwa wanapata baridi ya wastani tu wakati huu wa majira ya baridi.
Maafisa wameamua kufunga mashule ili watoto wabaki salama kutokana na baridi kali, ambayo inaweza kupelekea vidole kukatika katika dakika chache kama ngozi ikiachwa wazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment