Watu
waliokuwa wakifanya shopping katika supermarket ya Walmart iliyoko
Tewksbury, Marekani jana usiku (Dec 20) walikuwa surprised kumuona
superstar Beyonce aliyefika katika supermarket hiyo kufanya shopping ya
sikukuu, na kikubwa zaidi alinunua album yake ya mpya ambayo sasa
inapatikana katika maduka ya kawaida.
Beyonce akiangalia cd za album yake mpya baada ya kuanza kuuzwa rasmi
Kipenzi
cha Jay Z, Queen Bey alishare picha hizo katika ukurasa wake wa
facebook na kuandika ‘A little shopping today at Walmart. #BEYONCÉ is
available now in store.’
Mwimbaji
huyo wa ‘Crazy in love’ ameonekana akinunua nakala ya Cd ya album yake
mpya ‘Beyonce’ ambayo tayari imeanza kuuzwa katika CD. ‘Beyonce’ ilitoka
rasmi alhamisi iliyopita kwa kushitukiza na kuanzwa kuuzwa kupitia
iTunes exclusively kwa muda wa wiki moja.
Beyonce akilipia CD ya album yake aliyoinunua mara baada ya kuingia rasmi sokoni
Katika
shopping hiyo Queen Bey ametumia $37,500 (Milioni 59 Tshs) kwaajili ya
manunuzi ya zawadi za Christmas, na kuwazawadia watu waliokuwemo katika
supermarket hiyo kadi za X-mas, kila moja ikiwa na thamani ya $50
iliyoandikwa “Happy Holidays from Beyonce.”
No comments:
Post a Comment