15 December 2013

SHUGHULI YA MAZISHI YA MZEE NELSON MANDELA HIVI SASA KIJIJINI QUNU

Kamera ya Globu ya Jamii ipo Ndani ya Hema maalumu ambamo shughuli ya mazishi ya marehemu Nelson Mandela inaendelea hivi sasa katika kijijini Qunu.Na kama ilivyo ada ya libeneke la Globu hili kwamba halilali na litakuwa linakuletea Live matukio yote yanayoendelea katika Mazishi ya Shujaa huyo wa Afrika na Dunia kwa Ujumla.
Rais Jakaya Kikwete akitoa historia fupi ya Marehemu Mzee Nelson Mandela kuhusiana na mahusiano aliyokuwa nayo na Tanzania.
 Rais Jakaya Kikwete ni mmoja wa viongozi mbalimbali wanaoshiriki kwenye mazishi ya hayati Mzee Nelson Mandela yanayofanyika leo kijijini kwao Qunu, nchini Afrika Kusini.
Watu wengi maarufu Duniani wapo eneo hili hivi sasa kuhudhuria mazishi ya Mzee Nelson Mandela yanayoendelea hivi sasa katika kijiji cha Qunu,baadhi yao ni Oprah Wilfrey,Forest Whitaker,Richard Branson,Idris Ebra na wengine wengi.
Mwili wa Mzee Mandela ukiwasili ukumbini.
Rais wa Zamani wa Zambia,Mzee Keneth Kaunda pia yupo.
Ankal akisalimiana na Mcheza Filamu,Idris Elba ambaye amecheza Filamu ya Long Walk to Freedon inayoelezea mapambano ya Mzee Mandela wakati alipokuwa akihangaika kuutafuta uhuru wa mtu mweusi nchini Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname