Katika mahojiano na gazeti hili, mzee huyo ambaye ni mfugaji, Nzije Shanga Komite (58) alisema sasa hana tena mpango wa kuoa kwani umri umekwenda na hawezi kuhimili mikikimikiki ya ndoa mpya.
“Nina wake 12 na watoto wengi tu hata siwakumbuki majina na wengine wamepata wenzao wanajitegemea,” anasema Komite ambaye baada ya kupatiwa elimu ya ufugaji wa kisasa, alivuna sehemu ya mifugo yake na baada ya kuiuza, amefanikiwa kujenga nyumba ya kulala wageni ambayo pia ina sehemu ya biashara ya baa, amenunua gari la kutembelea, trekta kwa ajili ya kilimo cha kisasa.
Aidha, licha ya kuanza kufurahia maisha ya kisasa huku akibakiwa na ng’ombe zaidi ya 1,000, anasema bado ana safari ndefu ya kutaka kuyafikia malengo yake, akisema kwa sasa anasaka pesa kwa udi na uvumba aweze kujenga nyumba ya kuishi yeye na familia yake, badala ya kung’ang’ania kwenye nyumba ya tembe.
Kwa habari zaidi usikose kusoma hapa kwenye tovuti
No comments:
Post a Comment