MATOKEO DARASA LA SABA: Watahiniwa 411,127 wafaulu kujiunga sekondari
Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa
kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya
sekondari katika shule za Serikali.
Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na
serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na
elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.
Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya
sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini
amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza
halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya
madarasa hadi ifikapo machi mwaka mwakani.
Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.
Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na
mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa
vyumba vya madarasa 412.
Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za
msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa
na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment