14 October 2013

WATANZANIA TUMESHAURIWA KUMUENZI MWALIMU NYERERE LEO KWA KUUCHUKIA UHARIFU...


Watanzania wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu  Julius Nyerere kwa kuchukia uhalifu na kuhakikisha taifa linaendelea kuwa la amani, usalama na utulivu  kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera Senso  alisema hayo wakati akizungumza na mpekuzi  wetu  kuhusu maadhimisho ya leo ya Siku ya Nyerere.
 

 Senso alisema Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi mwenye msimamo imara, alichukia vitendo  vyote vya ubadhirifu, unyanyasaji, uchochezi wa kidini, kisiasa ikiwa ni  pamoja na vitendo vya uhalifu.
 

Wakati huo huo maadhimisho ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanafanyika kitaifa leo mjini Dodoma yakiongozwa na mwanasiasa mkongwe, Balozi Job Lusinde. 

Mkurugenzi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Charles Magaya alisema itaongozwa na mmoja wa washirika wa Baba wa Taifa, Balozi Job Lusinde.
 

"Maadhimisho hayo yataongozwa na mmoja wa washiriki wa Baba wa Taifa katika kupigania Uhuru wa Tanganyika Mheshimiwa Balozi Lusinde ambaye pia ni muasisi wa Chama cha TANU," alisema Magaya.

Sambamba na maadhimisho hayo, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeandaa sinema mbalimbali za Mwalimu Nyerere zitakazooneshwa katika viwanja vya Nyerere Square.

Magaya aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kushiriki katika maadhimisho hayo ya kumuenzi Baba wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname