Baadhi
ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma ambao Raia wa kigeni leo
wamejikuta katika hali ya simanzi na majonzi baada ya kukutana na wenzao
ambao wapo college tofauti , wanafunzi hao walijikuta wamekutanishwa
kwa pamoja bila kutegemea baada ya Ambassador wa NMB maarufu kama Team
kicollege pluS kuwakutanisha na kuwapa elimu juu ya huduma za NMB, ishu
ilikuwa ni baadhi ya wanafunzi hao Raia wa kigeni ambao wapo college
ya social waliomba ambassador wa NMB kuwapeleka
wanafunzi hao ili
waungane na wenzao ambao wapo college ya Tiba
(medicine) na kupewa elimu juu ya huduma za NMB ila hali ilikuwa tofauti
baada ya wanafunzi kuwaona wenzao kwanza hawakuamini na pili walijikuta
katika hali ya kuangua kilio kwa madai ya kwamba wanafunzi wa kibongo
wanawatenga na kuwanyanyapaa na tena huwa wanajisikia vibaya kwa sababu
ya kwamba wanahisi kunyanyapaliwa kwa sababu wapo nchi ambayo siyo
yao..... kiukweli raia hao hawafamu lugha ya kiswahili na pia kingereza
chenyewe ni cha magumashi lkn linapokuja swala la kuwatenga siyo ishu
kabisa . Na walikuwa wanatia huruma sana kwa jinsi walivyokuwa
wanaelezaa,Pia ambassadar wa NMB walijikuta katika kazi ya ziada ya
kuwabembeleza na kutatua swala hilo kwa kuwaahidi kulipeleka kwa uongozi
wa chuo hicho:TAZAMA VIDEO HAPO CHINI JINSI ILIVYOKUWA LEO HII CHUONI
HAPO: |
No comments:
Post a Comment