17 October 2013

PICHA:RIHANNA AVUNJA REKODI AFRIKA KUSINI KWA KUUJAZA UWANJA WA MPIRA KATIKA ''DIAMOND WORLD TOUR''


Ile idadi ya watu ambao hufurika katika mechi kubwa za mpira hasa za kimataifa ndiyo ambayo Rihanna aliweza kuikusanya huko Afrika Kusini Jumapili iliyopita. Rihanna
Weekend iliyopita star wa Barbados aliileta ‘Diamonds World Tour’ Africa, na mashabiki jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini ndiyo waliobahatika kuwa wa kwanza kushuhudia show kali ya hits zake mbalimbali nchini humo.
Mwimbaji wa ‘Diamonds’ Riri amevunja rekodi katika show hiyo ya uwanjani baada ya tiketi zote kuisha kitu ambacho mtandao wa Entertainment Wise unadai hakijawahi kutokea kwa show ya uwanja wa mpira.
Riri-SA
Kwa mujibu wa mtandao wa huo tiketi zote za show hiyo zilimalizika na zaidi ya watu elfu 67 walihudhuria katika show hiyo ya uwanjani na kumfanya Rihanna kuvunja rekodi kwa kuwa msanii mdogo zaidi wa kike wa kwanza kujaza uwanja wa mpira na tiketi zote kuisha.
Hilo lilikuwa ni jambo la mafanikio hata kwa RiRi mwenyewe ambaye alishare habari hizo

kwa kutweet “Rihanna’s show tonight in South Africa will be one of the biggest audiences ever for a female artist and the youngest ever to sellout the stadium.”
Na baadaye alitweet, “Sold out stadium show in #Johannesburg !!! Over 67’000 people #Jah. #histoRIH,”
Rihanna bado yuko Afrika Kusini anakotegemea kutumbuiza jijini Cape Town kesho (October 16)
Tazama baadhi ya picha za Rihanna akiwa ametembelea Zoo nchini humo
Ri-Sa2 Ri-Sa1 Ri-Sa3 Ri-Sa5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname