Produza Kameta akiwa kwenye studio yake TIKA Production
Produza Kameta ambaye alifanya kazi na
Mr Nice kipindi ambacho msanii huyo anaanza muziki amesema kuwa
msanii huyo anahitaji msaada hivi sasa na si wakati wa
kumlaumu.Produza huyo ambaye alifanya album ya kwanza ya Mr Nice
'Kidalipo' iliyokuwa na nyimbo kama 'Kikulacho', 'Kidalipo' na
nyingine ambazo ndo nyimbo zilizomtambulisha msanii huyo kipindi
hichi kwenye ramani ya muziki Tanzania.
Mr Nice alipata nafasi ya kupata
mkataba katika studio za GrandPa Rec zilizoko nchini Kenya lakini
mkataba wake ulisitishwa baada ya GrandPa kutangaza kuwa msanii huyo
ni msumbufu na hafanyi kazi kwa muda kutokana na kunywa pombe
nakusahau muda wa kazi.Baadae msanii huyo alichukuliwa na lebo
nyingine ya huko Kenya Candy n Candy lakini hivi sasa inasemekana
msanii huyo yuko Tanzania baada ya kushindwa kufanya kazi na lebo
hiyo.
Produza huyo alisema yeye binafsi
amefanya juhudi za kumtafuta msanii huyo kwa njia ya simu lakini
namba aliyonayo haipatikani mpaka leo..MSIKILIZE hapo chini;
No comments:
Post a Comment