Muimbaji mkongwe wa
muziki Tanzania, Zahir Ali Zorro ameungana na Ian Mbugua wa Kenya na
muimbaji Juliana Kanyomozi wa Uganda kama majaji wa Tusker Project Fame,
msimu wa 6.
“Tanzanian music legend
Zahir Ali Zoro joins the #TPF6 judging team. He’ll be one of the judges
alongside @IanMbugua and @JKanyomozi,” kimeandika kituo cha runingo cha
Citizen TV cha Kenya kinachorusha mashindano hayo.
Zahir Zorro ni baba mzazi wa wanamuziki Banana na Maunda Zorro.
Mwanamuziki huyo mkongwe amechukua nafasi ya Hermes Lyimo aka Hermy B aliyekuwa jaji kwa misimu kadhaa ya shindano hilo.
Hata hivyo, kuchukuliwa kwa Zorro kama jaji wa shindano hilo, kumepokelewa kwa hisia tofauti huku wengi wakionesha kutomkubali.
Hizi ni baadhi ta tweets kumhusu #JudgeZorro.
Hata hivyo si wote wanaomdhihaki:
Source: Bongo5
Source: Bongo5
No comments:
Post a Comment