18 October 2013

Dj Choka kuwapa 'Deal' wasichana watatu wanaojua kurap vizuri lakini hawajatoka.

Dj Choka amesema kuwa ameona kwenye ngoma zake wanahitajika wasichana wengine wanaoweza kuchana, huku akipigia mstari uwezo wa wasichana hao(wawe wakali).
 “Nafikiria tena kufanya ngoma na wasichana wanaorap lakini wakali, yaani nataka nikipata wawili lakini wawe wanarap ile yenyewe yani, haijalishi Kiswahili au kiingereza. Unajua kwenye ngoma zangu mi naona namuweka tu Vanessa Mdee, unajua Vanessa anaimba lakini akija kwenye project yangu inabidi achane.” Amesema Dj Choka.
Kuhusu sifa na jinsi ya kuwapata wasichana hao, alifunguka, “nafikiria kufanya Ki-search kidogo hivi lakini ntawaambia kwa kuwa bado ni mapema, nataka kufanya search ndogo tu ili nipate wasichana kama watatu hivi ambao watakuwa wanarap,ntafanya search siku si nyingi tu halafu ntawapata hao, kwa hiyo wakae mkao wa kula .”
Dj Choka hivi sasa anapika project yake anayofanya na wasanii kadhaa wenye umri mdogo na tayari Young Dee, M-Rap, Janjaro na Country Boy wameshaweka vocal ndani ya studio za BHitz, lakini Dj amesema zipo project nyingine zitakazotangulia kutoka kabla ya project hiyo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname