02 October 2013

BABA WA MAREHEMU MAC 2 B AFUNGUKA NA KUSEMA KUA MADAWA YA KULEVYA NDO YALIPELEKEA HADI MTOTO WAKE KUFARIKI



 Baba wa msanii MacMalick katikati akihojiwa
Baba wa marehemu MacMalick ambaye alikuwa msanii wa kundi la Wateule, Mzee Said Mohamed amesema kuwa matumizi ya madawa ya kulevya ni janga la Taifa.Mzee huyo alisema kuwa kipindi ambacho mtoto wake anatumia madawa ya kulevya hakujua mapema.Na pale alipokuja kugundua anasema kuwa ilikuwa ni 'too late'.
Mzee huyo alisema kuwa madawa ya kulevya ni vita ya jamii nzima na si kuilaumu Serikali, “watu wanapenda kupata pesa za haraka,na pia watu wanapenda kuwalaumu wazazi kuchangia kwenye madawa ya kulevya kwa kuwadekeza watoto lakini si kweli”, alisema Mzee

Baba alieleza kuwa kama mzazi hakufurahia hali hiyo na alitumia sehemu ya pato lake kumhudumia na kumsaidia hadi pale Mwenyezi Mungu alipomchukua

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname