Harufu ya rushwa! Safu ya ulinzi katika maduka ya biashara ya Mlimani
City, Dar kwenye geti la kuingilia na lile la kutokea, inadaiwa
kutawaliwa na rushwa ambapo walinzi wamenaswa ‘laivu’ wakipokea
‘mlungula’.
Kwa mujibu wa walalamikaji, walinzi hao wanadaiwa kujiwekea utaratibu
usiyo rasmi chini ya kampuni ya ulinzi wa eneo hilo iliyotajwa kwa jina
la Omega Nitro Risk Solutions ya jijini Dar ambapo ‘vijana’ wake
wanatuhumiwa kutoza watu faini ya shilingi elfu kumi kwa gari ambalo
mhusika wake amepoteza kadi ya kuingia na kutoka.
Madai hayo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kumekuwa hakuna
utaratibu mahususi kwenye ishu hiyo kwani baadhi ya walinzi kila mmoja
hujiamulia kuchukua fedha bila mhusika kupewa risiti ya malipo.
“Kuna tatizo kwenye safu ya ulinzi, huwa tunatozwa faini shilingi elfu kumi ukipoteza kadi,” alisema mmoja wa walalamikaji hao.
Baada ya malalamiko kutua kwenye kitengo chetu cha Oparesheni Fichua
Maovu (OFM), kazi ilianza ambapo kikosi kazi kilifanya doria kwa siku
kadhaa na kufanikiwa kunasa laivu hatua kwa hatua, tukio la walinzi hao
wakilamba ‘kitu kidogo’.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika geti la Mlimani City la
upande wa Barabara ya Sam Nujoma ambapo walinzi hao walizuia gari la
jamaa aliyekuwa amepoteza kadi na kuchukua rushwa.
Katika hali ya kushangaza au njaa, tofauti na kiasi cha shilingi elfu
kumi kilichotajwa awali, walinzi hao walikubali kumpunguzia jamaa huyo
hadi elfu tano bila kujua kwamba walikuwa wakirekodiwa hatua kwa hatua.
Baada ya kujikusanyia ushahidi wa kutosha, OFM ilizungumza na bosi
wao ambaye ni Senior Inspector wa Omega Nitro Risk Solutions, Leo John
Masuka juu ya vitendo hivyo ambapo mbali na kuonesha kushangazwa na
habari hizo, pia alianika kila kitu jinsi wanavyofanya kazi.
“Nashangaa kama kuna tatizo kama hilo kwani tumesitisha kuwatoza
faini wanaopoteza kadi, nitafanya uchunguzi ili kuwabaini watu hao ambao
wanaharibu sura ya kampuni.
Katika hali hiyo kwa kipindi hiki cha tishio la ugaidi ni rahisi kwa
magaidi kutoa rushwa kisha kuingia na kufanya utekaji kama walivyofanya
nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment